-
DAYS
-
HOURS
-
MINUTES
-
SECONDS

Dhibiti Kisukari Tumia AfyaPlan Application

Ninaweza kukusaidia kudhibiti kisukari

Elimu sahihi
Ratiba bora wa vyakula
Tathmini
+
Niliowasaidia
Waliodhibiti
%
Mafanikio

Si Huduma ya Kawaida ya Kudhibiti Kisukari

MloPlan si huduma nyingine ya kupanga chakula; ni mshirika wako kamili katika kusimamia kisukari. Kwa mipango ya chakula iliyobinafsishwa, upatikanaji wa ushauri wa wataalamu, na zana za kisasa, MloPlan inaweka kiwango kipya katika huduma ya kisukari

Si ushauri wa kawaida wa biashara mtandaoni. Tuko na wewe nyumbani! Unaweza kushauriana kwa wakati unaokufaa, na pia kuwa na vikao na tathmini maalum na Dr. Adinan. Muhimu zaidi, tunakuletea chakula unachokipenda. Hakuna sheria, ni mipango tu.

Kutana na Dr. Adinan

Dr. Adinan J. ni mtaalamu wa afya aliyejitolea kabisa kwa kutoa huduma inayomlenga mgonjwa. Anajulikana kwa kuwa mtu anayefikika na anayeelewa,

Dr. Adinan huchukua muda wa kusikiliza wasiwasi wa kila mgonjwa na kubinafsisha matibabu ili yakidhi mahitaji yao ya kipekee. Kama mtafiti, Dr. Adinan yupo mstari wa mbele katika maendeleo ya tiba, akiendelea kutafuta njia bunifu za kuboresha matokeo ya wagonjwa.

Dr. Adinan

Namna ninavyokusaidia Ufanikiwe!


Furahia Vyakula Vyako:
Tunaelewa umuhimu wa kufurahia chakula chako. Programu yetu inakusaidia kupanga milo yako kwa usahihi, ili uweze kuendelea kufurahia vyakula vyako bila kuathiri afya yako. Tofauti na hospitali zinazotoa ushauri wa jumla, MloPlan inakusaidia kila wakati, kuhakikisha unaweza kufurahia milo yako.

01

Msaada wa Kina:

Hatupatii tu ushauri; tunakusaidia kuunda na kufuata mpango unaokufaa. Wataalamu wetu wanashirikiana na watoa huduma wako wa afya kuhakikisha mpango wako wa kudhibiti kisukari unafanikiwa.

02

Taarifa Sahihi:

Katika enzi inayoshughulika na taarifa nyingi za afya, ni muhimu kuwa na data za kuaminika. Tunatoa elimu inayothibitishwa na tafiti, ikusaidie kufanya maamuzi sahihi. Utapata makala, punguzo kwenye vitabu, na ushauri wa wataalamu ili kuepuka habari potofu.

03

Kuzuia Madhara:

Kudhibiti kisukari siyo tu kuhusu kudhibiti viwango vya sukari bali pia kuzuia madhara. Jifunze kuhusu vifaa muhimu kama monofilament kwa ajili ya kupima mishipa ya fahamu—ambavyo mara nyingi vinapuuziliwa mbali lakini ni muhimu. Tutakuongoza jinsi ya kutumia vifaa hivi kwa ufanisi ili kuepuka matatizo makubwa ya afya.

04

Huduma Binafsi

Kinyume na ushauri wa jumla, programu yetu inatoa huduma zilizobinafsishwa. Kutoka tathmini ya awali hadi msaada wa mara kwa mara, tunabinafsisha kila kitu kulingana na mahitaji yako, kuhakikisha unafahamu hali yako na jinsi ya kudhibiti kwa ufanisi.

Tunafanya hivi

Unapojiunga na KisukariPlan unakuwa mstari wa mbele kwenye kuboresha afya yako. Hii ni huduma shirikishi. Moja kwa moja tunaanza kupanga vitu pamoja

01

Tathmini ya Awali:

Mara tu unapojiunga, utapokea tathmini ya kina kuhusu hali yako ya kiafya, mapendeleo ya chakula, na malengo ya afya.

02

Mrejesho na Malengo

Tutakaa pamoja na kutoa mrejesho kuhusu hali yako ya afya. Pia tunapanga malengo ambayo tutayapitia pamoja kila wiki.

03

Mpango Binafsi wa Mlo

Kulingana na tathmini yako, tutakutengenezea mpango wa mlo maalum unaolenga kuboresha kudhibiti kisukari na shinikizo la damu, pamoja na kuboresha afya yako kwa ujumla.

04

Elimu Sahihi

Ili usikufuate mkumbo, unahitaji kuelewa ugonjwa wa kisukari kwa uhakika. Tutakupa elimu sahihi kupitia vitabu, video, sauti, na maandiko kwenye tovuti yetu. Hatutajizuia kwa kula tu; wataalamu wetu watakufundisha hadi namna ya kuandaa chakula chako.

05

Ushauri na Msaada wa Mara kwa Mara

Utapokea ushauri wa kila wiki kutoka kwa wataalamu wetu, ikiwa ni pamoja na mapitio ya mlo wako, marekebisho ya mpango wa mlo, na msaada wa kutathmini tiba. Pia utakuwa unaweza kuweka miadi na daktari kwa wakati unaokufaa.

06

Ushirikiano na Wenzako Wanaodhibiti Kisukari

Ikiwa unataka, unaweza kujiunga kwenye jukwaa letu na kushiriki katika majadiliano na wagonjwa wenzako. Majadiliano haya yana malengo mawili:

Kujifunza kutoka kwa wenzako waliozishinda changamoto unazokabiliana nazo.
Kuwasaidia wenzako kukabiliana na changamoto mbalimbali.

07

Vifaatiba Muhimu

Wagonjwa wengi wanaodhibiti kisukari wana vipimo nyumbani kufuatilia hali yao ya afya. Kuwa na kipimo hukusaidia kufahamu hali yako ya sukari, hivyo kuthibitisha ufanisi wa matibabu

Wanavyosema waliojiunga!

Dhibiti kisukari na Boresha Afya yako na Dr.Adinan

Jiunge sasa

Scroll to Top