Kisukari ni Nini?
Kisukari ni ugonjwa wa kimetaboliki ambao husababisha viwango vya sukari katika damu kuwa juu zaidi ya kiwango cha kawaida.
Huu ugonjwa unapotokea, mwili hauwezi kutumia sukari (glucose) kwa ufanisi, ambayo inaweza kuathiri jinsi unavyojisikia na hata kupelekea matatizo mengine ya kiafya.
Dhibiti Kisukari
Kwa mara ya kwanza tunakusaidia kudhibiti kisukari kupitia ushauri wetu wa kitaalamu usiojali umbali uliopo kati yako na daktari
Kisukari ni Ugonjwa Gani?
Kisukari, au ugonjwa wa kisukari, ni ugonjwa sugu ambapo mwili hawezi kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu.
Mwili hushidnwa kudhibiti sukari kwasababu ya matatizo katika utendaji wa insulini, homoni inayosaidia kuingiza sukari kwenye seli za mwili kutumika kama nishati au kuihifadhi.
Ingawa wengi hufahamu aina mbili za kisukari, ukweli ni kwamba aina za kisukari si kama meno ya tembo – ziko zaidi ya mbili.
Aina za Kisukari
- Kisukari Aina ya Kwanza (Type 1 Diabetes): Hii ni aina ya kisukari ambapo mwili hauwezi kutoa insulini kutokana na uharibifu wa seli za kongosho. Kisukari aina ya kwanza mara nyingi hutokea kwa watu wenye umri mdogo.
- Kisukari Aina ya Pili (Type 2 Diabetes): Aina hii hutokea wakati mwili hawezi kutumia insulini ipasavyo au hutoa insulini kwa kiasi kidogo. Kisukari aina ya pili mara nyingi huathiri watu wazima na inahusishwa na uzito kupita kiasi na mtindo wa maisha usio bora.
- Kisukari cha Mimba (Gestational Diabetes): Hutokea wakati wa ujauzito na huweza kupona baada ya kujifungua. lakini wanawake wenye kisukari cha mimba wana hatari kubwa ya kupata kisukari aina ya pili baadaye maishani.
- Kisukari kinachotokana na magonjwa mengine, mfano ugonjwa wa matezi kwenye figo na kwenye mayai ya uzazi ya mwanamke. Magonjwa haya husababisha kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Lakini yanatibika na hivyo aina hii ya kisukari hutibika.
Madhara ya Ugonjwa wa Kisukari
Kisukari kinapototolewa bila udhibiti, kinaweza kusababisha madhara mbalimbali kama vile matatizo ya moyo, kushuka kwa kiwango cha kuona, magonjwa ya figo, na matatizo ya vidole kama vile vidonda vinavyochelewa kupona.
Pia, inaweza kusababisha uharibifu wa mishipa ya damu na neva.
Kisukari Husababishwa na Nini?
Kisukari husababishwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na:
- Mabadiliko katika Genetiki: Historia ya familia inaweza kuongeza hatari.
- Mtindo wa Maisha: Uzito kupita kiasi, kutoza mazoezi, na ulaji wa chakula chenye mafuta mengi.
- Matatizo ya Kinga: Katika kisukari aina ya kwanza, mfumo wa kinga huweza kushambulia seli za kongosho zinazozalisha insulini.
Matibabu ya Kisukari
Matibabu ya kisukari hujumuisha:
- Matumizi ya Dawa: Dawa za kupunguza viwango vya sukari kwenye damu.
- Mabadiliko ya Lishe: Kula vyakula vyenye kiwango kidogo cha sukari na mafuta, na kuongeza ulaji wa matunda na mboga.
- Mazoezi: Kufanya mazoezi mara kwa mara ili kusaidia mwili kutumia sukari vizuri zaidi.
- Monitoring: Kudhibiti viwango vya sukari mara kwa mara kwa kutumia glucometer.
Namna ya Kudhibiti Kisukari
- Kufuatilia Kiwango cha Sukari: Pima sukari yako mara kwa mara ili kujua jinsi inavyojirekebisha.
- Kula Vyakula Bora: Jumuisha vyakula vyenye virutubisho vingi na epuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta.
- Kufanya Mazoezi: Tafuta shughuli za mwili zinazokufaa na zipige mara kwa mara.
- Kushirikiana na Wataalamu: Pata ushauri kutoka kwa madaktari au wataalamu wa afya kuhusu jinsi ya kudhibiti hali yako.
Jali afya yako kwa kuchukua hatua za kudhibiti kisukari mapema na kwa ufanisi. Kwa ushauri zaidi na mpango wa kudhibiti kisukari, tembelea KisukariPlan.