Huduma ya kudhibiti Kisukari kutoka AFYATech
Dhibiti Kisukari, Ishi kwa amani
Elimu sahihi, huduma shirikishi, na utayari : Njia zilizothibitishwa kudhibiti kisukari
Tunawahudumia wahitaji ambao
- Wanataka msaada wa moja kwa moja kudhibiti kisukari – Tutakufundisha kuanzia sababu, dalili, matibabu hadi namna ya kudhibiti na kuepuka madhara
- Unaamini kisukari hakina tiba kwasasa ila unaweza kuidhibiti na kwamba ushirikiano kati yake na mtaalamu wa afya utafanikisha udhibiti wa kisukari
- Utayari wa kuchukua hatua stahiki kwa wakati: kudhibiti kisukari na kuepuka madhara yake tutakushauri hatua zote muhimu za kuchukua kutathmini ugonjwa wako na hatua za kuchukua
KisukariPlan ikoje?
Tumeandaa mchakato maalum utakaohakikisha kama unafanikiwa kudhibiti kisukari na kukurudishia amani
Dhibiti Kisukari Plan
Fahamu
Fahamu yote kuhusu kisukari
- Ushauri wa jumla kila wiki kwenye majukwaa yetu mtandaoni.
- Kusoma makala zote kuhusu kisukari na presha na magonjwa mengine kwenye tovuti yetu
- *Vipimo muhimu kufuatilia na kudhibiti kisukari ukiwa nyumbani kwa bei ya punguzo
MloPlans
Maamuzi sahihi baada ya kutathmini tiba
- Huduma zote kwenye mpango wa Fahamu, na
- Uchambuzi wa vyakula na Ratiba / Mpango wa chakula kulingana na vyakula unavyovipenda kwa wiki
- Ushauri mahususi wa namna ya kuepuka madhara ya kisukari ikiwemo kufanyiwa tathimini ya tiba
Ushauri
Ongea na Daktari wako
- Kuongea na Dr. kwa muda wako, na
- Ushauri mahususi kulingana na swali utakalo uliza
- Kusoma makala zote kuhusu kisukari na presha na magonjwa mengine kwenye tovuti ya AFYATech
- Punguzo la vitabu na vifaatiba utakavyohitaji
Tunajua ufanisi wa huduma hii. Tumeitoa tangu 2016.
Fikiria, kwa miaka 15 sasa! Wakati wote huu nilikuwa ninatumia dawa. Kwakweli sukari yangu ilikuwa sawa angalau 5 mpaka 6 lakini nilikuwa namiss sana vyakula vyetu, unajua tena Zanzibar. Lakini kwa kuzingatia kiasi kama ulivyo elekeza, sasa ninakula vyakula hadi vile vya wanga bila kuathiri kisukari.
nilikuwa naiga kula kama wagonjwa wengine wanavyokula, lakini sukari yangu bado ilikuwa si chini ya 10. Baada ya kufuata muongozo wa kupanga ratiba ya vyakula kwenye kitabu, kama ulivyoelekeza sasa daktari nimefanikiwa vyote. Naweza kupanga ratiba ya vyakula, kupanga kiasi na kuchanganya vyakula vizuri. Sasa sukari yangu iko 6.5.