Kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari, kipimo cha kisukari (glucometer) ni kipimo muhimu sana, kinachotoa kinachopima kiwango cha sukari mwilini. Kipimo cha sukari ni muhimu kufanikisha udhibiti wa kisukari.
Chaguo sahihi la glucometer linaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika ufanisi wa kusimamia kisukari. Katika makala hii, tutachunguza mambo muhimu ya kuzingatia unapohitaji glucometer bora kwako.
Kipimo cha Kisukari (Glucometers) nini Nini?
Glucometer, au inayojulikana kama glucose meter, ni kifaa cha matibabu kinachobebeka kiurahisi ambacho hutumika kupima kiasi cha sukari mwilini.
Kifaa hiki kinachunguza sampuli ya damu ambayo mtu huitoa kwa kujichoma – mara nyingi kidole.
Kwa kawaida, kipimo cha kisukari huja katika seti inayojumuisha
- kipimo cha kidigitali cha sukari kinachotumia
- betri,
- sindano ndogo (lancets),
- kifaa cha kuchomeka sindano kinachoweza kurekebishwa kulingana na unene wa ngozi,
- vifaa vya upimaji, na
- kitu cha kurekodi kumbukumbu ya mwenendo wa kisukari – inaweza kuwa mfumo maalum wa kidigitali au kitabu cha kumbukumbu ya sukari mwilini
Kipimo cha Kisukari Kinafanyaje Kazi?
Vipande vya upimaji vina kemikali maalum ya sukari inayochakata sampuli ya damu. Kifaa hichi kupitia kemikali hii na kifaa cha kompyuta huweza kusoma na kutoa majibu ya sampuli.
Faida za Kuwa na Kipimo cha Kisukari
Wagonjwa wa kisukari aina ya 1 na 2, pamoja na kisukari cha mimba wakati wa ujauzito. Kwa kufuatilia viwango vya sukari mwilini, unapata ufahamu wa jinsi lishe na mazoezi vinavyoathiri viwango vya sukari, na kuruhusu mtoa huduma wa afya kubuni mpango wa matibabu uliotengenezwa kwa ajili yako.
Aina za Kipimo cha Kisukari?
Kuna aina mbili kuu za mita za sukari:
- Mita za Sukari za Kawaida:
- Zinafaa kwa watu ambao hawahitaji kupima mara kwa mara au sindano za insulin.
- Hupima sukari mwilini kwa kutumia sampuli ya kidole kwenye kipande cha upimaji kilichowekwa kwenye kifaa.
- Kinachopima Sukari wakati wote:
- Kpimo hichi huwafaa ziaidi wagonjwa wa kisukari aina ya 1, wale ambao wanahitaji ufuatiliaji wa karibu wa kiwango cha sukari, wagonjwa waliokwenye insulin pump na wale ambao huwa hawapati dalili za kupungukiwa na sukari au wale ambao kiwango cha sukari hupungua sana au huongezeka sana mara kwa mara.
- Kipimo hiki hakiitaji sindano kwani kinabandikwa kwenye ngozi
- Kipimo hiki cha sukari cha kuendelea hutoa majibu ya wakati husika na hivyo kukifanya kuwa kipimo sahihi kwa kutambua kiwango cha sukari muda wowote.
Pima Kisukari Kwa Usahihi
Fahamu kiwango cha sukari kwenye damu yako na chukua hatua stahiki mapema unapotumia kipimo cha kisukari chenye teknolojia ya hali ya juu.
Faida za Glucometers
Kuwa na kipimo cha sukari kuna faida mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
- Kusaidia kufikia malengo yako ya sukari mwilini.
- Kupunguza ziara za dharura hospitalini kwa sababu ya kisukari kupanda.
- Kusaidia katika kudhibiti sukari mwilini kwa muda mrefu, ambayo hupunguza hatari ya matatizo kama ugonjwa wa moyo, matatizo ya figo, na matatizo ya macho.
- Kutoa taarifa muhimu ambazo unaweza kutumia kuwasiliana na tabibu wake, na hivyo kurahisisha matibabu.
Jinsi ya Kutumia Kipimo cha Kisukari – Glucometer
Kutumia glucometer inaweza kuonekana kuwa ngumu mwanzoni, lakini inakuwa rahisi baada ya mazoezi.
Kwa glucometer ya kawaida, fuata hatua hizi zinazopendekezwa na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC):
- Hakikisha kifaa cha kupimia sukari ni safi.
- Chukua kipande cha upimaji (Strips) na kufunga mara moja chombo cha upimaji ili kuzuia uharibifu wa hewa kuingia kwenye kichupa kinachohifadhi.
- Osha na kausha mikono yako, na minya kidole kwa upole ili kuongeza mtiririko wa damu.
- Tumia sindano (lancet), iliyojumuishwa katika mfuko wa glucometer, kuchoma kidole chako kwa kina kinachofaa kulingana na unene wa ngozi yako. Tumia sindano safi na mpya kila wakati.
- Weka strips kwenye kifaa cha kupimia sukari. Hakikisha ile sehemu yenye kama waya ndo imeingia.
- Weka tone la damu kwenye sehemu ya mbele ya strips. Baada ya sekunde chache, matokeo yako yataonekana, kawaida kwa mg/dL au Ml/L (miligramu ya sukari kwa desilita ya damu).
- Rekodi matokeo yako kwenye kitabu cha kitabu au mfumo wa kifaa, pamoja na maelezo kuhusu mambo yoyote ambayo yanaweza kusababisha matokeo yako kutokuwa tofauti na ulivyotegemea, kama vile vyakula ulivyokula hivi karibuni au shughuli yoyote.
- Tupa sindano na kipande cha upimaji sehemu salama.
Matumizi ya kipimo cha kisukari kinachopima wakati wote, huitaji mtaalamu kukiweka.
Waya wa kifaa unawekwa chini ya ngozi, na kushikiliwa kwa kutumia kifaa maalum.
Mtumaji mara nyingi hupokea majibu kupitia simu ya mkononi baada ya kipimo hiki kuunganishwa na program ya simu.
Hatahivyo kwa mara ya kwanza / siku za mwanzo unaweza bado kuhitaji kuthibitisha matokeo kwa kutumia glucometer ya kawaida.
Kutafsiri Matokeo ya Kipimo cha Kisukari
Unapojua kiwango chako cha sukari mwilini, ni muhimu kujua kina maana gani.
1. Kipimo cha sukari masaa 2 baada ya kula – mtu huwa na kisukari kama kiwango cha sukari kwenye damu yake ni kikubwa zaidi ya 11 mmol/L
2. Kipimo cha sukari wakati mtu hajala ndani ya masaa 6. Mara nyingi hupimwa asubuhi kabla mtu hujala chochote – mtu huwa na kisukari kama kiwango cha sukari kwenye damu yake ni kikubwa zaidi ya 7 mmol/L
Offer ya Muda Mfupi!
Pata Punguzo la TSh. 50,000/=
Kipimo cha Presha Na Kisukari

- Fuatilia sukari yako ukiwa nyumbani
- Fahamu kama tiba inafanya kazi
- Fahamu nini husababisha sukari kupanda
- Kuwa na amani
Mambo 5 Ya Kuzingatia Unapochagua Glucometer Bora Kwako
Unapochagua glucometer, kuna mambo mengi ya kuzingatia, ikiwa ni pamoja na:
- Urahisi wa Kutumia: Zingatia mambo kama kasi ya kupata matokeo, ukubwa wa kifaa, na mara ngapi unahitaji kupima.
- Ufanisi: Kipimo cha maabara ni fanisi zaidi ya glucometer za kawaida na CGMs. Pia, vipimo hivi vya kisukari hutofautiana majibu kati ya kampuni tofauti. Hivyo ni muhimu kuzingatia kwamba vipimo vimeidhinishwa na mamlaka husika.
- Teknolojia: Pia ufanisi huathiriwa na teknolojia inayotumika kupima kiwango cha kisukari. Kuna vipimo vingine ambavyo hutumia teknolojia ya hali ya juu kiasi cha kuweza kupima kiwango cha sukari hata pale kiwango cha damu kinapokuwa kidogo. Mfano wa kipimo chenye ufanisi wa hali ya juu.
- Bei: Glucometer za kawaida zinaweza kugharimu kati ya TSh. 35,000/= hadi zaidi ya dola TSh. 200,000/=, lakini kumbuka gharama za vipande vya upimaji (stripes). Kipimo cha wakati wote mara nyingi ni ghali zaidi.
- Upatikanaji: Je kipimo cha kisukari na vya kupimia (stripes) zinapatikana sehemu kubwa ya mazingira yako? Ni muhimu kuhakikisha hili ili usishindwe kufuatilia kiwango chako cha sukari.
Udhibiti wa kisukari unategemea kwa kiasi kikubwa utumiaji sahihi wa kipimo cha kisukari / glucometer kulingana na mahitaji yako maalum na mtindo wa maisha.
Fanya uchaguzi wa kufahamu kwa kuzingatia vipengele, usahihi, gharama, upatikanaji na teknolojia unapochagua glucometer bora katika mapambano yako na ugonjwa wa kisukari.