Mazoezi ni sehemu muhimu ya kudhibiti kisukari, lakini si mazoezi yote yana athari sawa kwa mgonjwa wa kisukari.
Kuna aina mbili kuu za mazoezi—anaerobic na aerobic—na zote zina faida tofauti kwa afya yako.
Kuelewa tofauti kati ya aina hizi na jinsi zinavyoathiri viwango vya sukari kwenye damu ni muhimu kwa mtu yeyote anayetaka kudhibiti kisukari kwa ufanisi.
Tofauti Kati ya Mazoezi ya Anaerobic na Aerobic
Kama unafikiri hujui mazoezi ya aerobic, ukweli ni kwamba unayajua vizuri na huwenda unayafanya.
Kila unapokuwa unatembea, kukimbia taratibu au kuendesha baiskeli, unafanya mazoezi ya aerobic!
Faida za mazoezi ya aerobic kuboresha afya ya moyo, yanaongeza kasi ya mwili kuchoma kalori, husaidia kupunguza uzito, kushusha shinikizo la damu, kuongeza kiwango cha HDL (cholesterol “nzuri”) na kuboresha afya ya akili.
Lakini vipi kuhusu mazoezi makali? Unapojitahidi kufikia kiwango cha juu kabisa cha juhudi zako, unabadilika kutoka mazoezi ya aerobic kwenda kile kinachojulikana kama mazoezi ya anaerobic.
Wakati wa mazoezi ya aerobic, oksijeni inaweza kufika kwenye misuli yako (ndiyo maana kuna “aero” katika aerobic), lakini si hivyo katika anaerobic.
Kila aina ya mazoezi ya mwili inayofanywa kwa kiwango cha nguvu ambacho hakiwezeshi oksijeni kufika kwa kiasi cha kutosha kwenye misuli ni anaerobic.
Oksijeni siyo tofauti pekee kati ya mazoezi ya aerobic na anaerobic. Mwili wako pia hutumia njia tofauti za kuzalisha nguvu. Unapofanya mazoezi ya aerobic mafuta na sukari hutumika kama chanzo cha nishati.
Ukifanya mazoezi ya anaerobic—kama vile mbio za kasi—mwili hutoa glycogen (aina ya sukari) kutoka kwenye misuli ili kutumika kama nishati.
Kukosekana kwa glycogen kwenye misuli na kuongezeka kwa asidi ya lactic wakati wa mazoezi ya nguvu ya anaerobic ni sehemu ya sababu inayosababisha misuli yako kuchoka haraka na maumivu baada ya mazoezi.
Jinsi Mazoezi ya Anaerobic Yanavyoongeza Kiwango cha Sukari Mwilini
Ingawa mazoezi kwa ujumla yanasaidia kupunguza viwango vya sukari kwenye damu, mazoezi ya anaerobic yanaweza kufanya mambo kuwa tofauti kidogo.
Wakati wa mazoezi ya anaerobic, mwili unahitaji nishati ya haraka, ambayo inasababisha ini kutoa glukosi kwa kasi ili kutoa nishati kwa misuli.
Kwa hivyo, kwa wagonjwa wa kisukari, mazoezi ya anaerobic yanaweza kusababisha viwango vya sukari kuongezeka kwa muda mfupi baada ya mazoezi.
Kiwango cha sukari kinapanda baada ya mazoezi
Usiogope! Hii ni athari ya kawaida, na kwa kushirikiana na daktari wako au mtaalamu wa afya, unaweza kujua jinsi ya kudhibiti hali hii.
Kiwango cha sukari kinaweza kuongezeka mara moja, lakini mara baada ya mwili kuzoea zoezi hilo, mabadiliko haya yanakuwa yasiyodhuru.
👉 Unahitaji msaada wa kibinafsi wa kudhibiti kisukari chako kupitia mazoezi na lishe? Pata ushauri wa kitaalamu kupitia programu yetu ya KisukariPlan. Angalia huduma yetu hapa.
Kuongeza Mazoezi ya Anaerobic Katika Ratiba Yako
Kunyanyua uzito ni njia nzuri kwa watu wa viwango vyote vya mazoezi kuongeza mazoezi ya anaerobic kwenye ratiba yao.
Mazoezi ya nguvu yanaimarisha udhibiti wa viwango vya sukari kwenye damu na kusaidia mwili kutumia insulini kwa ufanisi zaidi. Pia hupunguza mafuta mwilini, huongeza misuli, na kuimarisha nguvu za mwili.
Watu wenye kisukari wanapaswa kulenga kufanya mazoezi ya nguvu kwa wiki angalau mara tatu.
Ili kuongeza mazoezi ya nguvu hakikisha unapata ushauri kutoka kwa daktari kwanza!
Ikiwa unahitaji msaada wa kibinafsi wa kupanga ratiba yako ya mazoezi na lishe, huduma zetu za MloPlan zitakusaidia kudhibiti kisukari kwa njia bora. Angalia zaidi hapa.
Ukishapata ushuari, nakuelekeza kubadilisha vipindi virefu vya mazoezi ya kiwango cha wastani na vipindi vifupi vya mazoezi ya nguvu.
Kwa kuanza tumia angalau dakika moja kwenye mazoezi ya nguvu nyingi.
Kwa mfano, tembea au kimbia kwa mwendo wa kawaida kwa dakika tatu hadi tano, kisha ongeza mwendo kadri uwezavyo kwa sekunde 30 hadi 60. Rudia mpangilio huu mara mbili au tatu.
Polepole ongeza muda wa kubadilisha viwango vyako vya nguvu wakati wa mazoezi badala ya kufanya mazoezi kwa kiwango cha wastani tu.
Kadri unavyofanya zaidi ya vipindi hivyo, mwili wako huanza kuzoea, na huwa rahisi zaidi.
Utafiti unaonyesha kuwa kufanya mazoezi ya namna hii huimarisha kiwango chako cha usawa wa mwili kwa haraka zaidi kuliko kufanya mazoezi kwa kiwango cha wastani kwa muda mrefu.
💡 Faida: Mbali na kuimarisha misuli na mifupa, mazoezi ya anaerobic pia yanaweza kuboresha afya ya akili, kuongeza ujasiri, na kukusaidia kudhibiti uzito.